Mgombea wa kiti cha ubunge katika eneo la Kitui Magharibi, Ben Muasya anazidi kuimarisha ushawishi na umaarufu wake mbele ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 , huku wagombea wengine wakionekana kutia breki katika azma zao za kuwania wadhfa huo.

Muasya, ambaye anafahamika pakubwa kutokana na uwezo wake wa kusaidia makundi mbalimbali katika eneobunge hilo kujiendeleza na kuboresha maisha yao, atawania kiti hicho kupitia tikiti ya chama cha UDA kinachoongozwa na Naibu rais William Ruto.

Kampeni za kinyang’anyiro hicho zinaendelea kushika kasi, huku mbunge wa sasa Bi. Edith Nyenze akilazimika kutafuta mbinu mbadala ili kustahimili makali ya Benedict Muasya.

Kulingana na kura ya maoni, Muasya anaongoza kwa asilimia 54, Nyenze akichukua nafasi ya pili kwa asilimia 41 huku wagombea wengine wakijinyakulia asilimia 5 ya uwezekano wao kuibuka washindi katika kivumbi hicho.

See also  Revealed Why Ngilu Want to Face Malombe than Musila or Kiema in 2022

Facebook Comments Box